• Breaking News

    Serikali kuboresha TBC


    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo NAPE NNAUYE amesema serikali iko katika mkakati wa kuliboresha Shirika la Utangazaji Tanzania - TBC
    Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Tablet tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa Kagera
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo NAPE NNAUYE amesema serikali iko katika mkakati wa kuliboresha Shirika la Utangazaji Tanzania - TBC kwa kulipa uwezo wa ushindani dhidi ya vyombo vya habari vya ndani na vile vya kimataifa.

    Waziri NAPE ameyasema hayo katika mkutano wa pamoja na wadau wa sekta ya habari mkoani KAGERA katika ziara yake ya siku moja mkoani humo.

    Waziri NAPE ametoa agizo kwa Halmashauri zote nchini kutoa mamlaka kamili kwa maafisa habari na kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi

    Katika mkutano huo baadhi ya maafisa habari kutoka wilaya tano za mkoa wa Kagera  wamekabidhiwa vitendea kazi aina ya ipad huku wadau mbalimbali wakitoa ushauri juu ya namna ya kuboresha sekta ya michezo, sanaa na utamaduni pamoja na tasnia ya habari kwa ujumla.

    Na Charles Mwebeya
    15 April 2016

    No comments

    Post Top Ad