• Breaking News

    OBAMA asifu majeshi yake yanayopigana na IS


    Rais BARACK OBAMA amedai kuwa majeshi ya nchi yake, yanayoongoza mapambano dhidi ya wapiganaji wa kikundi cha IS nchini IRAQ
    Rais BARACK OBAMA
    Rais BARACK OBAMA amedai kuwa majeshi ya nchi yake, yanayoongoza mapambano dhidi ya wapiganaji wa kikundi cha IS nchini IRAQ, yamekuwa yakiendesha oparesheni zenye mafanikio nchini na ghasia mpya kuanza nchini SYRIA.


    OBAMA amesema katika miezi michache iliyopita wapiganaji wa kikundi cha IS wamekuwa na wakati mgumu katika nchi hizo mbili.
    OBAMA amesema majeshi ya nchi yake, yakishirikiana na nchi washirika 66, na muungano wa nchi za kiarabu yamekuwa na ari kubwa ya kupambana na wapiganaji wa IS katika nchi za IRAQ na SYRIA. Amesema wapiganaji wa kikundi hicho wamejikuta katika kipindi kigumu, kwani wamekuwa wakipata mashambulio kutoka kila upande.
    OBAMA amesema majeshi hayo yameendelea kuwateka viongozi wa ngazi za juu wa kikundi cha IS na kuharibu ngome zake kuu katika maeneo hayo.

    April 14, 2016
    NYAMBONA MASAMBA

    No comments

    Post Top Ad