Habari ya Waziri Mwakyembe Yaliponza Gazeti la Mwanahalsi
Katika toleo namba 387 la Jumatatu April 17-23, 2017 gazeti la MwanaHalisi katika ukurasa wake wa kwanza lina habari isemayo: “Mwakyembe: Maisha Yangu Yako Hatarini.”
Habari
hiyo inadai kuwa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hayuko huru na maisha yake bado yapo
hatarini, taarifa ambayo imemshtua na kumhuzunisha sana Waziri kwa
uzushi, ulaghai na uzandiki uliopitiliza.
Mwandishi
wa habari hiyo amedai kufanya mahojiano na Dkt. Mwakyembe nje ya
viwanja vya Bunge mjini Dodoma Alhamisi iliyopita, na amenukuu kile
anachodai ni Waziri kueleza wasiwasi kuhusu usalama wa maisha yake, kitu
ambacho hakikutokea.
Tunapenda
kuutaarifu umma kuwa, habari hiyo ni ya uongo na ya kutunga. Mhe. Dkt.
Mwakyembe hajafanya mahojiano yoyote na mwandishi yeyote katika siku na
mahali palipotajwa sembuse mwandishi husika wa gazeti la MwanaHalisi
ambalo Mhe. Mwakyembe ana kesi nalo Mahakama Kuu kwa kumzushia habari za
uongo alipokuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Wakati
Serikali ikitafakari hatua za kuchukua kwa uandishi wa aina hii, tasnia
ya habari inaendelea kukumbushwa kuzingatia weledi na maadili hasa
wakati huu ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya
2016, tasnia ya habari imepewa hadhi ya kuwa taaluma kamili.


No comments