TIC Yazindua Kitengo Cha Huduma Za Mahala Pamoja Ambapo Huduma zote za uwekezaji Zitapatikana sehemu moja
Idadi
ya siku na utaratibu unaotumika kuomba vibali vya uwekezaji nchini
Itapungua baada ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kufungua huduma ya
mahala pa kutolea huduma za pamoja.
Katika huduma hiyo vibali kutoka taasisi zote zinazohusika na uwekezaji nchini zitapatikana katika sehemu moja.
Waziri
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ndiye aliyefungua
kituo hicho jijini Dar es Salaam jana ambapo katika maelezo yake
alizitaka taasisi za umma kufanya kazi kwa ushirikiano ili kupunguza
urasimu usio wa lazima na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara.
Awali
akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw.
Clifford Tandari alisema wao kama kioo cha wafanyabiashara wanaokuja
kuwekeza nchini wamejipanga kuhakikisha kuwa huduma wanazotoa
zinachochea ukuaji wa uchumi kama yalivyo matarajio ya serikali.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Bw.
Godfrey Simbeye aliipongeza hatua hiyo ya serikali na kwamba inaonesha
matumaini ya kufikia uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 25 katika
kipindi cha miaka mitano ijayo.
Waziri
wa Viwanda na Biashara ,Charles Mwijage, akizungumza na baadhi ya watoa
huduma katika Kitengo hicho mara baada ya uzinduzi wake.


No comments