Wahariri wataka muda zaidi muswada wa habari
Dar es Salaam. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imeomba muda
zaidi wa wadau kujadili muswada wa sheria ya huduma kwa vyombo vya
habari ili upelekwe bungeni February 2017.
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Theophil Makunga amesema muda wa mwezi mmoja waliopewa kuujadili hautoshi na na muswada huo si wa viongozi wa TEF pekee, bali unahusu maslahi ya wadau waliopo nchi nzima.
Amesema kama kamati ya Bunge itaupeleka muswada huo bungeni wiki hii kama ilivyoahidi basi hautakuwa umeshirikisha wadau.
Ameomba miezi miwili ili wadau nchi nzima waweze kuujadili na kutoa maoni kwa kuwa una kasoro nyingi ambazo zinatakiwa kujadiliwa.
Juzi, Kamati ya Bunge ya Huduma za jamii ilisema itaendelea na mchakato wa kujadili muswada huo ikidai baadhi ya wadau hawakujitokeza.

No comments