Kocha wa timu ya taifa ya Uganda,
Milutin Micho amesema, haziongopi timu za Ghana, Mali na Misri ambazo
zimepangwa pamoja katika kundi D katika fainali za kombe la mataifa ya
Afrika AFCON 2017 ambazo zitafanyika nchini Gabon mwakani.
Micho amesema, atajipanga kuhakikisha
timu yake inafanya vyema katika mashindano hayo na kuuwakilisha vyema
ukanda wa Afrika mashariki, CECAFA katika mashindano.
Kundi A lina timu za Gabon, Burkina
Faso,Cameroon na Guinea Bissau, wakati kundi B lenyewe lina Algeria,
Tunisia, Senegal na Zimbabwe Timu ya Taifa ya Ivory Coast itapambana na
kocha wake wa zamani Herve Renard baada ya kupangiwa katika kundi moja
na Morocco, Togo na DR Congo katika michuano ya fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika.
No comments