• Breaking News

    JINSI YA KUPATA WINDOW 10 KWA URAHISI



     Je wewe ni mtumiaji wa windows7 au windows8? na je  unajua kuwa waweza kupata windows 10 kutoka kwenye windows7 au windows8 unayo tumia? yah  hii inawezekana na ni rahisi sana.
         leo nipo hapa ili kukuelekeza nini ufanye ili uweze kupata windows10 tena ikiwa full activated kupitia windows 7 au windows 8
     kama unatumia windows 7 au wndows 8 ili kupata windows 10  kutoka hapo inabidi ufanye kitu kinacho itwa WINDOWS UPGRADE
      Kabla ya kufanya hivyo hakikisha kuwa windows unayo tumia ipo activated  na pia ipo updated.  pia hakikisha unajua kama computer yako ni 32bit au 64 bit. hii itakusadia kuweza kupata window10 inayoendana na computer yako
    ( kama window yako ikiwa updated itakuletea notfication ikikutaka ua upgrade kwenda kwenye windows10. )
     

     
      kama haikuletei waweza ingia hapa kupata installer ya window 10 ambayo itakusaidia  ku upgrade kutoka windows7 au windows8 kwenda windows10

      baaada ya kupakua hiyo installer unacho takiwa kufanya ni kuifungua/kuirun hiyo installer kwenye computer yako.
     kisha bonyeza palipo andikwa  ugrade this PC now  alafu bonyeza next



     utatakiwa kukubali kila kitakacho kuja katika set up yako ya windows10 kwa kubonyeza neno next, kuweka tiki au kubonyeza neno accept

     

     Baada kumaliza hapo itafata hatua za muhimu itakuja hatua nyingine ambayo ni hatua ya kudownload windows 10 kwenye computer yako

      ANGALIZO
    Hakikisha upo kwenye internet ambayo ni imara na pia hakikisha una kifurushi cha kutosha maana windows10 ina ukubwa wa zaidi ya 3GB.
       
     Ikishamaliza kudownload itaanza kuinstall kama inavyo onekana kwenye picha hapa chini



     Hakikisha unachagua keep personal files and apps hii itasaidia windows 10 kubakisha personal files na apps zako. kwamaana hiyo kila ulichokuwa unacho kabla ya ku upgrade kitabaki kama kilivyokuwa awali.


      ukimaliza bonyeza next ili windows10 iingie kwenye computer yako. na iache hadi imalize kuingia. pc yako ita reboot mara kadhaa ili kuinstall windows10. usiizime iache ikimaliza itajizima na kujiwasha yenyewe tena

    ikisha maliza ku UPGRADE itakuletea hatua nyingine ya mwisho ambayo itakuwa inahusu kufanya setting za mwisho ili uanze kutumia windows10 yako hii ni kwa sababu ni mara yako ya kwanza kuitumia windows10



    Bonyeza " use Express Settings" kisha itafunguka page kama inavyo onekana hapo chini. weka setting kama zinavyo onekana hapo chini kisha bonyeza next

     

    Ukibonyeza next itafunguka nyingine kama ilivyo hapo chini. na yenyewe jaza kama inavyo onekana hapo chini. kisha bonyeza next



    Baada ya hapo itakuja page nyingine ya mwisho ambayo inaonesha  Default apps, hapa unaweza kubadilisha  app ambayo unataka uitumie kwenye video,audio,photo au kuingilia kwenye internet
      windows 10 inakuja na Default app zake kama zinavyoonekana hapo chini, lakini zinaweza kubadilishwa na kuweka za kwako. cha kufanya ili kubadili bonyeza app husika ili kuibadili.



    Ukimaliza hapo bonyeza next ili kumaliza na kuanza kuitumia window yako.
       ikimaliza itafunguka kama inavyo onekana hapo chini


    Ili kuhakikisha zaidi anza kuziangalia apps zako kama zipo zote. fanya hivyo kwa kuzifungua moja baada ya nyingine.
     kumbuka windows 10 inakuja bila ya baadhi ya driver mfano VGA. hivyo ukishamaliza kuinstall hakikisha
    unaupdate windows10 ili idownload baadhi ya driver ambazo zimekosekana kisha ikimaliza kuziingiza restart computer yako.
       hizi driver haziwezi kupatikana kwa kutumia driver pack itakulazimu tu ku update window yako. na pia unapo upgrade windows10 yako inakuja ikiwa activated. hii ni kwasababu ulitumia window ambayo ni active kupata windows 10. so inatumia zile activation key za windows 7 au 8 kuji activate

     ENJOY YOUR WINDOWS10

    No comments

    Post Top Ad