• Breaking News

    Bodi ya mikopo kufanya uhakiki wa wanafunzi

    Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) imesema itaanza uhakiki wa taarifa za wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo ili kujiridhisha kama wanasifa sitahiki na ambao watakuta hawana sifa watasitishiwa mkopo.

    Mkurugenzi wa mtendaji wa HESLB,  Abdul-Razaq Badru amesema zoezi hilo litaanza Jumanne na wanafunzi wote watatakiwa kujaza dodoso ambalo litatolewa ambalo litawekwa kwenye mtandao wa bodi hiyo.

    "Lengo letu ni kujiridhisha kama wanaonufaika wote  kweli wanamahitaji sanjali na kuhakiki orodha yetu upya, katika hilo wale ambao hadhi zao zitaonesha kuwa sio wahitaji watapoteza sifa za kendelea kunufaika na  mkopo," alisema

    No comments

    Post Top Ad