Wizara ya nishati na madini yaanza kupokea maoni ya wananchi
Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewataka watanzania kutoa maoni yao yatakayoboresha utekelezaji wa miradi ya Rea
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa SOSPETER MUHONGO
Akizungunza jijini Dsm Profesa Muhongo amesema Wizara ina zaidi ya shilingi Trillion 1 ambayo inatakiwa kutumika katika miradi ya Rea hivyo maoni hayo yatasaidia utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha amesema kuwa maoni hayo yatafanyiwa tathmini na Wakandarasi,wafanyakazi wa Rea pamoja na wale wa Tanesco ili kupata taarifa sahihi na namna ya kutekeleza miradi hiyo na kufahamu changamoto zilizojitokeza katika miradi iliyotangualia.
Amefafanua kuwa Awamu ya tatu ya miradi ya Rea iko katika hatua za mwisho ili kuanza kutekelezwa na itahusisha vijiji vipya pamoja na vile vijiji vyote vilivyoachwa katika awamu ya kwanza na ya pili kwa sababu mbalimbali.
Amesisitiza kuwa watanzania wote waache tabia ya kulalamika na balaaa yake watumie fursa za kufikisha matakwa yao kwa kutoa maoni pale wanapopata nafasi.
Amesema maoni hayo yatolewe kupitia Sanduku la posta la Wizara, barua Pepe ambayo wataanza kufanyiwa kazi wakati wa sikukuu ya 7 7.

No comments