• Breaking News

    Waislamu waadhimisha Idd el fitri

    Waislamu nchini hapo leo wanaungana na wenzao duniani kusherekea siku kuu ya IDD EL FITRI baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan


    Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti, ABUBAKAR ZUBERI
    Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti, ABUBAKAR ZUBERI amesema Mwezi umeandama na kuonekana katika maeneo mengi ya nchi hapo jana
    Sikukuu ya EID inafanyika baada ya waumini wa dini ya Kiislamu kukamilisha ibada ya funga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni utekelezaji wa nguzo ya NNE ya dini ya kiislamu.
    Kitaifa swala ya Eid imefanyika katika viwanja vya MNAZI MMOJA jijini DSM huku baraza la EID litafanyika viwanja vya Karimjee.
    Mkururugenzi Mkuu Wa Shirika La Utangazaji Tanzania kwa niaba ya wafanyakazi wote wa shirika hilo anawatakia waislamu na watanzania Siku Kuu Njema ya EID EL FITRI.

    No comments

    Post Top Ad