WAPANDA PIKIPIKI KUNDI LILILO KATIKA HATARI ZAIDI.

Geneva: Takribani watu 1.25 milioni hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani kila mwaka. Hii ni kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani katika ripoti yake ya Usalama barabarani ya mwaka 2015 iliyotolewa tarehe 19/10/ 2015.
"Ajali za barabarani zinaongezeka maradufu, hususan kwa watu masikini katika nchi masikini" Amesema Dr Margaret Chan, mkurugenzi mkuu wa shirika la Afya Duniani.
Ripoti hiyo inaainisha kuwa, hatari kwa
watumiaji wa barabara ni tofauti kulingana na eneo mtu analoishi. Pengo kubwa ni dhahiri kati ya nchi zenye kipato kikubwa na zile zenye kipato cha chini na cha kati. Asilimia 90 (90%) ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani hutokea katika nchi zenye kipato cha kati na chini pamoja na kuwa na asilimia 54 tu ya vyombo vya usafiri duniani. Barani ulaya kuna idadi ndogo ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani, na bara la Afrika likiongoza kwa idadi kubwa ya vifo kwa mwaka.
Pamoja na hayo yote pia kuna nchi zilizofanikiwa kupunguza ajali na vifo na mafanikio haya yametokana na kuwa na sheria nzuri za usalama barabarini ambazo zinatekelezwa ipasavyo na kuzifanya barabara na vyombo vya usafiri kuwa salama.
Ripoti hiyo inasema kuwa nchi zaidi zinachukua hatua kuimarisha usalama barabarani. Katika miaka mitatu iliyopita, nchi 17 zimetilia mkazo wa angalau sheria moja ya sheria zake za usalama barabarani na hii imeonekana katika ufungaji wa mikanda ya magari,udhibiti wa unjwaji wa pombe wa madereva, udhibiti wa mwendo kasi, uvaaji wa kofia ngumu( helmet) kwa wapanda pikipiki na usalama wa watoto.
Tahadhari zaidi ni kwa kundi lililo katika hatari kubwa, ambalo ni wapanda pikipiki, ambalo linahusisha mpaka 23% ya vifo vyote vya ajali za barabarani. Katika nchi nyingi ajali za pikipiki zinaongezeka ambapo barani Amerika vifo vya wapanda pikipiki vimeongezeka kutoka 15% hadi 20% kati ya mwaka 2010 na 2013.Huko kusini mashariki mwa Asia na Magharibi ya Pasifiki, robo tatu ya vifo hutokana na ajali za wapanda pikipiki.
Waenda kwa miguu na wapanda baiskeli ni kundi la walio katika hatari wawapo barabarani. "Kuimarisha usafiri wa umma pamoja na usalama wa waenda kwa miguu na wapanda baiskeli, kutawezekana kwa kuangalia kwamapana jinsi ya kuboresha miundo mbinu na mgawanyo wa matumizi ya barabara. Kutokuwepo kwa sheria za kuyalinda makundi yaliyo katika hatari kunasababisha vifo kwa raia na kuiathiri miji. Tukizifanya barabara salama kwa waenda kwa miguu na wapanda baiskeli ni dhahiri kutakuwa na idadi ndogo ya vifo, shughuli za kiuchumi zitaimarika,tutapunguza uchafuzi wa mazingira na kuwa na majiji bora ya kuishi." Alisema Dr Etienne Krug, Mkurugenzi wa WHO wa kitengo cha magonjwa yasiyo ya uambukizi.
Sababu nyingine iliyotanabaishwa katika ripoti hiyo ambayo huchangia ajali ni ubora wa magari yaagizwayo kutoka ughaibuni.Ripoti hiyo imeonyesha kuwa, magari yaliyouzwa katika 80% ya nchi zote duniani hayakukidhi ubora wa usalama wa magari hayo, hususan katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.

No comments