• Breaking News

    Rais Magufuli amteua Mathias Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan

    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
    Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.
    Taarifa iliyotolewa leo tarehe 18 Aprili 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Chikawe umeanza tarehe 13 Aprili, 2016.

    Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo tarehe 15 Februari, 2016.

    Mheshimiwa Chikawe aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo Ia Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika serikali ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

    Gerson Msigwa
    Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
    Dares salaam

    No comments

    Post Top Ad