Simba watibua sherehe za Ushindi wa Yanga
Baada
ya kuenea kwa tetesi kuwa Klabu ya Simba imewasilisha malalamiko ya
barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupinga kunyang'anywa
pointi 3, hatimaye uthibitisho wapatikana.
Kitendo
cha Simba kuwasilisha rufaa hiyo na kuenea kwa picha ikionyesha
vielelezo hivyo, imeanza kuwakwaza mashabiki wa Yanga ambao walikuwa
wameanza sherehe za ubingwa.
Baadhi ya mashabiki wa Yanga, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwakejeli Simba kwa kuwaita “Wazee wa pointi za mezani”.
Simba imeamua kwenda Fifa kuhakikisha inapata pointi tatu ambazo kama itafanikiwa, basi moja kwa moja itatangazwa kuwa bingwa.
Haya
ni baadhi ya maneno aliyoandika Msemaji wa Simba aliyefungiwa, Haji
Manara;....."Last week nilipowapongeza Yanga kwa ushindi na kuwaambia
mapambano yanaendelea,sijui kama tulielewana!! Bila shaka sasa
mmenielewa, soon tutapewa haki yetu,MWANA KULITAKA,MWANA KULIPEWA"
Halafu
akaendelea;........"Hv unadhani FIFA wana figisu guys?kadi tatu za
njano ni kukosa game inayofuata tu,no way out!!ukizingatia repoti za
mwamuzi na kamisaa na bodi inayosimamia ligi, sasa mjiandae kisaikolojia
kulileta kombe kwa magoti!SHUBAMIT"
No comments