Wizara yatenga Sh18.1 bil kujenga mahakama
Serikali
kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka 2017/18 imetenga Sh18.1
bilioni kwa ajili ya kujenga na kukarabati mahakama mbalimbali nchini.
Kauli
hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki
alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Mlalo,
Rashid Shangazi(CCM).
Shangazi
alihoji ni lini Serikali itakarabati majengo machakavu ya Mahakama ya
Mwanzo Mtahe iliyopo kwenye Jimbo la Mlalo mkoani Tanga.
Kairuki
alisema azma ya Serikali ni kusogeza huduma za mahakama karibu na
wananchi na kwamba katika mwaka wa fedha 2016/17 zilitengwa Sh 46.5
bilioni ambazo zimefanya kazi kubwa.
Alisema
mahakama ambazo zipo kwenye utaratibu wa kukarabatiwa ni Mahakama Kuu
ya Tanga na Dar es salaam na kuanza ujenzi katika Mahakama Kuu ya Mara
na Kigoma.
Katika
swali la msingi la Mbunge wa Njombe Mjini (CCM), Edward Mwalongo
alitaka kujua kama Serikali itakuwa tayari kukarabati Mahakama za Mwanzo
za Mahenye na Igomonyi ili wananchi waweze kupata huduma hiyo karibu.
Akijibu
swali hilo Kairuki alisema moja ya changamoto kubwa zinazoikabili
Mahakama ni uchakavu wa miundombinu na ukosefu wa majengo ya kutosha.
Alisema
mpango uliopo ni kujenga majengo mapya na siyo kukarabati yaliyopo hasa
ikizingatiwa kuwa majengo yaliyoombewa na mbunge yapo kwenye hifadhi za
barabara na pia ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Njombe ni miongoni mwa
miradi ya kipaumbele.
Kuhusu
Mahakama ya Mahenye alisema imeshapata nafasi katika Ofisi ya Kijiji
cha Uwemba kwa ajili ya kuendesha shughuli za Mahakama ya Mwanzo Mahenye
ili huduma iendelee kutolewa wakati mipango ya ujenzi inaendelea.

No comments