Serikali Yapokea Msaada wa Bilioni 490 Kutoka Umoja wa Ulaya za Miradi ya Maendeleo..!!!
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepokea msaada wa Sh490
bilioni kutoka Umoja wa Ulaya(EU), kwa ajili ya kufanikisha miradi ya
kilimo, afya na viwanda.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Doto James amesema maelekezo ya msaada huo ni sehemu ya mpango wa pili wa maendeleo wa serikali.
“Wametoa euro 205 sawa na Sh486.9bilioni na watazitoa katika kipindi cha
miaka minne kuanzia msimu huu wa bajeti, wanaanza kutoa
Sh120bilioni,"alisema James wakati wa kusaini makubaliano ya upokeaji wa
msaada huo.
"Serikali haipokei msaada bila utaratibu,kabla ya kuzipokea Kamati ya
kitaifa ya madeni inautazama na kutoa ushauri kwa serikali."alisema
No comments