Huu ndo Uwezo wa Korea Kaskazini Kivita....
Korea
kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti
ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani.
Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90.
Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti.
Hivi
karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa
marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo
yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi.
Taifa
la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi
ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13.
Makombora ya Hwasong yakiwa katika maonyesho
Ishara
za kwanza kuhusu utengenezaji huo ulifanyika Septemba 2016 ambapo taifa
hilo lilifanyia majaribio mashine mpya ya roketi ambayo baadhi ya watu
wanasema inaweza kurusha kombora kutoka bara moja hadi jingine.
Idara
ya ulinzi nchini Marekani Pentagon inaamini kwamba Korea Kaskazini
inamiliki makombora 6 aina ya KN-08, ambalo lina uwezo wa kufika hadi
Marekani.
Korea
kaskazini inaaminika kutengeza toleo jipya la kombora hilo
linalojulikana kama KN-14. Haahivyo makombora hayo hayajafanyiwa
majaribio.
Lakini
mnamo mwezi Januari 2017, kulikuwa na ishara ya jaribio, muda mfupi
baada ya kiongozi Kim Jong un kudai kwamba taifa hilo lilikuwa katika
awamu ya mwisho ya kutengeza kombora la masafa marefu linaloweza
kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
Mpango
wa kisasa wa kutengeza makombora yaa Korea Kasakzini ulianza kwa
kutengeza makombora ya scud ambapo yalipitia Misri mwaka 1976.
Kufikia 1984, taifa hilo lilikuwa likitengeza makombora yake kwa jina Hwasong.
Inaaminika kuwa na makombora tofauti tofauti ya masafa mafupi ambayo yanaweza kulenga taifa jirani la Korea Kusini.
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Korea umeharibika na yamekuwa yakijiandaa kukabiliana kivita.
Kombora
la Hwasong 5 na Hwasong 6 ambayo pia hujulikana kama Scud B na Scud C
yana uwezo wa kwenda kilomita 300 na 500 mtawalia kulingana na kituo cha
Marekani kinachofanya utafiti wa kuzuia kuenea kwa nuklia.
Makombora hayo yanaweza kubeba makombora ya kemikali na nyuklia.
Silaha hizo zimejaribiwa na kupelekwa katika maeneo yanayohitajika na kombora la Hwasong-6 limeuzwa nchini Iran.
Ramani ya Korea Kaskazini na majirani zake wa Korea Kusini
Korea
Kaskazini ilianza mpango huo mapema miaka ya 80 kutengeza kombora la
masafa ya kadri kwa jina Nodong likiwa na uwezo wa kusafiri urefu wa
kilomita 1000.
Kombora hilo limetengezwa kwa muundo wa Scud ,lakini ni asilimia 50 kwa ukubwa na lina mashine yenye uwezo mkubwa.
Uchanganuzi
wa mwezi Aprili 2016 wa taassii ya kimataifa kuhusu utafiti wa mikakati
,unasema kuwa makombora hayo yalithibtishwa yanaweza kupiga maeneo yote
ya Korea Kusini na Japan.
Imeongezea
kuwa maonyesho ya Oktoba 2010 yalithibitisha kuwa kombora hilo linaweza
kufika urefu wa kilomita 1,600 ikimaanisha kwamba linaweza kupiga kambi
kadhaa za Marekani zilizopo katika eneo la Okinawa.
Makombora hayo ya Nodong yanadaiwa kujaribiwa 2006, 2009, 2014 na 2016.
Kombora la Musudan
Korea Kaskazni imekuwa ikitengeza makombora ya Musudan kwa miaka kadhaa, na hivi karibuni ilifanya majaribio 2016.
Makadirio
yanatofautiana kuhusu viwango vyake, huku ujasusi wa Israel ukitaja
uwezo wake kuwa kilomita 2,500 nacho kitengo cha ulinzi wa makombora
nchini Marekani kikikadiria kuwa na uwezo wa kufika kilomita 3,200.
Duru nyingine zinasema kuwa kombora hilo lina uwezo wa kwenda kilomita 4,000.
Kombora
la masafa mafupi la Musudan ambalo pia linajulikana kama Nodong B ama
Taepodong-x linaweza kulishambulia taifa lote la Korea Kusini na Japan.
Kombora hilo linaweza kushambulia kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Guam.
Kombora la masafa marefu la Taepodong linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine
Korea
Kaskazini inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la masafa ya kadri,
kwa jina Pukguksong, mnamo mwezi Agosti 2016 likirushwa kutoka kwa
manuwari.
Kombora la pili lilirushwa kutoka ardhini mnamo mwezi Februari 2017.
Pyongyang
ilisema kuwa ilitumia mafuta ,na kufanya kuwa rahisi kuliwasilisha na
kurusha. Hatahivyo maelezo kuhusu uwezo wake hayajulikani.
Credit: BBC




No comments