Ningekuwa Diamond nisingejiita simba – Darassa
Hit maker wa wimbo ‘Muziki’
ameweka wazi maana ya ule mstari wake wa “sio simba, sio chui, sio
mamba” kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani simba ni mnyama
ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.
Darasa
amedai Diamond ni msanii ambaye amehangaika sana kutoka kimuziki hivyo
mafanikio yake na uwezo wake wa muziki alitakiwa ajiite jina lingine kwa
kuwa Daimondi ni zaidi ya Simba kwa sasa kwani ni zaidi ya mnyama
Simba.
“,”
alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Ninavyomuona Diamond ni zaidi
ya Simba, kuna watu wanaua simba, simba, kajichanganya, kaingia kijijini
kapotea, Diamond kwa kitu anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza
kujiita jina lingine lolote kubwa, kafanya vitu vingi sana,”
Pia
rapper huyo alidai wanyama wote ambao amewataja katika wimbo wake
hawaogopi kwa kuwa ana kitu kikubwa ndani yake na yeye ni mwanaume na
anajiamini kwa muziki wake anaofanya.

No comments