Lowassa atoa neno kwa waliomtabiria kifo
Waziri Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa, amesema kuwa Serikali ya
Chama cha Mapinduzi (CCM), ina watu wenye roho mbaya kwani waliwahi
kumuombea kifo,lakini hadi leo anadunda.
Lowassa ambaye alikuwa
mgombea urais wa Chadema na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi(Ukawa), amesema baadhi ya waliomwombea kifo leo
hawapo duniani,kwani mungu ndiye anayepanga maisha ya mwanadamu.
“Kule
kwa wenzetu kuna watu wenye roho mbaya,kwani hata mimi waliniombea
kifo,waliniombea kifo muda mrefu kweli lakini mpaka sasa bado nadunda tu
wakati baadhi ya walioniombea hivyo,leo hawapo duniani kwa mapenzi ya
mungu”alisema Lowassa.
Lowassa aliyasema hayo jana baada ya
wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa ufunguzi wa uchaguzi mdogo wa
udiwani kata ya Matevezi jimbo la Arumeru Magharibi,kupaza sauti
wakimuuliza juu ya hatima ya mbunge wao Lema ambaye yupo Gereza la
kisongo kwa miezi miwili sasa.
Katika hatua nyingine, Lowassa aliwataka timu ya kampeni na wananchi
kuhakikisha kura haziibiwi kwa kile alichoeleza kuwa Chadema ina nguvu.

No comments