Waziri Mkuu: Waliofaulu Ni Lazima Waende Sekondari
Kassim Majaliwa amesema Serikali haitavumilia kuona mamia ya vijana
waliofaulu mitihani ya darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha
kwanza wanabaki nyumbani eti kwa kuwa hakuna madarasa ya kutosha.
“Serikali
haitaridhika kuona vijana waliofaulu vizuri wanashindwa kwenda kidato
cha kwanza. Halmashauri zilijua tangu mapema ni wanafunzi wanaenda shule
za msingi kwa hiyo inataka kuona wote waliofaulu wanakwenda sekondari
kwa asilimia 100,” amesema.
Ametoa
kauli hiyo jana mchana wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa
mkoa wa Lndi mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu
ndogo wilayani Nachingwea. amewasili wilayani Nachingwea akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapunziko ya mwisho wa mwaka.
Alisema
Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutoa elimu ya bure kwa kila
mtoto sasa iweje watoto wengine wanafaulu na wanashindwa kujiunga na
elimu ya sekondari.
“Tumesema
elimu ni bure hakuna sababu ya kufanya wengine wasiende shule wakati
azma ya Serikali ni kutoa elimu ya bure. Hakikisheni wote wanaingia
katika chaguo la kwanza,” alisema.
Aliwataka
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo zimefaulisha
wanafunzi lakini hazina madarasa na madawati ya kutosha warudi mezani na
kujipanga upya ili kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanapangwa na
kuanza na wenzao katika chaguo la kwanza kwani wakisubiri chaguo la pili
wanakuwa wamechelewa.
“Kama
tumepokea vijana wengi kwenye udahili wa kidato cha kwanza, ni dhahiri
kuwa ,tutapata Vijana wengi watakaomaliza kidato cha nne. Sote tunajua
kuna agizo la kila tarafa kuwa na sekondari moja ya kidato cha tano na
sita, nataka utekelezaji wa agizo hili usimamiwe kuanzia sasa.”
“Tafuteni
moja kati ya shule kwenye tarafa zenu na ipandishwe hadhi kwa kuwekewa
miundombinu inayotakiwa ya bwalo, jiko, mabweni, mifumo ya maji,
madarasa na vyoo vya kutosha,” alisema.
Katika hatua nyingine,
alisema atafuatilia ili abaini ni kwa nini taasisi ya maghala ya
Serikali inadai tozo kwa wakulima wanaohifadhi mazao kwenye maghala
hayo.
alisema atapitia sheria ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ili kuona kama
inaruhusu tozo hizo na kuangalia sheria gani inawaruhusu kutoza kodi.
Alihoji inakuwaje taasisi ya Serikali inatoza tozo kwenye maghala ambayo
yamejengwa na wananchi.
Akitoa mfano kuhusu ghala la Liwale,
alisema: “Kuna viagency vimeanzishwa kazi yao ni kutoza mapato tu.
Inakuwaje kunakuwa na taasisi imekaa tu na kuanza kutoza tozo kwa
wananchi wanaotumia facility za Serikali. Sheria ya kutoza tozo
imetokana na nini na hizo zinakwenda kwa nani, je srikali imeanza
kufanya biashara?,” alihoji.
“Nimepata
taarifa kuwa walikuja kuzuia mazao yasitoke hadi wao walipwe, hapana
huu siyo utaratibu. Ni kwa nini tuwanyang’anye fedha wale waliojenga
ghala? Wao walijenga ghala kutokana na ubunifu halafu unasema unawapa
sh. 7/- kwa kilo wakati wewe umetoza sh.25/- kwa kilo moja. Hapana hilo
halikubaliki,” alisisitiza.
alisema kama Serikali inaruhusu kuwepo kwa tozo hizo kwa jambo ambalo
wananchi wamelibuni wenyewe, basi ilipaswa kudai kodi na hiyo kodi
ilitakiwa kukusanywa na Mamlaka ya mapato (TRA) na siyo vinginevyo.
alisema atafuatilia wakala mbalimbali walioanzishwa kwenye wizara kwani
kuna nyingine zinafanya kazi ambazo zilistathili kufanywa na idara
kwenye wizara mama.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA
No comments