Bodi ya Mikopo yawatosa Watanzania wanaosoma China
Watanzania
waliopata ufadhili wa kusoma nchini China, hawatapata mikopo baada ya
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuwaondoa kwenye
orodha ya wanufaika.
Taarifa iliyotolewa na HESLB, ikijibu Ubalozi wa
nchini China, kuhusu madai ya kuchelewa kwa fedha za mikopo kwa
wanafunzi wanaosoma nchini humo imeeleza kuwa hatua hiyo inatokana na
maelekezo ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwamba wanafunzi
wote wanaopata ufadhili kutoka nchi rafiki watajitegemea ikiwamo gharama
za tiketi za ndege.
Barua
hiyo ya Desemba 20, 2016 iliyomnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo,
Abdul Razaq Badru inaeleza kuwa mwaka huu wanafunzi hao hawatanufaika na
mikopo kama ilivyokuwa ikitolewa miaka ya nyuma.
Jana,
akizungumza na waandishi wa habari, Badru aliitambua barua hiyo huku
akisita kutolea ufafanuzi wake kwa madai ilikuwa ni majibu kwa wanafunzi
hao wa China.
Hata hivyo, alisema endapo kutakuwa na madai kutoka kwa wanafunzi hao watalazimika kutolea ufafanuzi.
Akizungumzia
suala hilo Naibu Waziri Elimu, Stella Manyanya alisema ni hekima zaidi
kuangalia au kusaidia wanafunzi wa ndani wasiokuwa nacho kuliko
wanaopata ufadhili wa nje ya nchi.
Advertiseme

No comments