• Breaking News

    DC Irando akutana na madudu kituo cha afya Tunduma

    Momba. Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma  Irando abaini utolewaji mbovu wa huduma za afya usiofuata utaratibu unaofanywa na wahudumu katika kituo cha Afya Tunduma.

    Irando akiongozona na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Ally Mwafongo pamoja na Ofisa wa Tarafa wa Mji wa Tunduma, Edward Lugongo alifika kituoni kumjulia hali mchezaji aliyeumia wakati mchezo wa ufunguzi wa michuano ya ligi ya kombe la Wilaya ya Momba kati ya Fc Zaragoza ya Mbeya na Fc Tunduma.

    Irando na viongozi aliongozana nao walilazimika kuwatafuta watoa huduma kwa dakika zaidi ya 45 baada ya kuwasuburi mapokezi kwa dakika 30 bila kupewa huduma pamoja na kuwepo kwa wagonjwa waliokuwa wakisuburi kusikilizwa eneo la mapokezi kwa kipindi kirefu.

    Dc Irando alipowahoji wagonjwa hao walikiri kutokusikilizwa kwa muda huo hali iliyomlazimu mkuu wa wilaya kuwafata wahudumu wodini, kuonyesha kuwa hawakuwa wakijuwa uwepo wa Mkuu wa wilaya kituoni hapo.

    No comments

    Post Top Ad