Waziri Muhongo : Serikali Ya Uganda Kujenga Kiwanda Cha Kuchakata Mafuta Ghafi Na Kuwa Safi
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema Serikali ya
Uganda itajenga Kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi na kuwa masafi
(refinery)katika eneo la Kabaale katika wilaya ya Hoima nchini humo.
Profesa
Muhongo amesema hayo baada ya kutembelea eneo hilo nchini Uganda wakati
wa vikao vya kujadili michakato ya ujenzi wa bomba la mafuta kutoka
Kabaale - Hoima nchini humo hadi katika bandari ya Tanga nchini
Tanzania.
Vilevile
amesema kuwa Serikali ya Uganda imetoa jumla ya 40% ya hisa za
(refinery) hiyo kwa Serikali 5 za Afrika Mashariki kabla ya Sudani
kusini kujiunga.
Katika
hisa hizo Tanzania imekaribishwa na kutengewa 8% za kununua hisa hizo
zenye thamani ya US$150.4 Millioni. Aidha Prof. Muhongo ameishauri
Serikali na Sekta Binafsi kushirikiana kununua hisa hizo.
Katika
hatua nyingine ujumbe wa Tanzania na ule wa Uganda juu ya ujenzi wa
bomba la mafuta umetembelea eneo la ziwa Albert na kujionea visima
vilivyochorongwa tayari kwa uzalishaji wa mafuta ghafi (crude oil).
Ambapo inakadiriwa kuwepo kwa mapipa bilioni 6.5 ya akiba (reserve) na yanoyoweza kuchimbwa ni mapipa bilioni 2 (recoverable).
Ujenzi
wa Bomba la mafuta kutoka Kabaale Uganda hadi Tanga (The East African
Crude Oil Pipeline ) utagharim dola za Marekani Bilioni 3.55 na litakuwa
na urefu wa kilometa 1,443, na litakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa
200,000 kwa siku.

No comments