ULAJI BROKOLI HUTUEPUSHA NA MAGONJWA HATARI.-UTAFITI.
Mboga aina ya brokoli |
Ulaji wa mboga aina ya brokoli (broccoli) waweza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa
hatari ya moyo, kisukari aina ya pili, pia aina mbalimbali za saratani. Dutu
zijulikanazo kama flavonoids katika vyakula hivi, husaidia mwili kuweza kupambana na maradhi hayo
hatari yanayotishia maisha ya walio wengi.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Illinois Marekani wanasema kuwa dutu za phenolic ni muhimu katika
"Watu walao mboga zenye kiasi kikubwa cha dutu hizo huwa na uwezekano mdogo wa kupata
maradhi hayo hatari" anasema Dr Jack Juvik wa kitivo cha sayansi ya vinasaba kutoka
chuo hicho. Anaendelea kusema kuwa, " kwa kuwa miili yetu haiwezi kutengeneza dutu hizo,
hivyo basi ni muhimu kuhakikisha kuwa tunakula vyakula vyenye virutubisho ili kuboresha
afya ya miili yetu".
Utafiti huo unahusisha sayansi ya vinasaba ili kuweza kuzalisha brokoli, kabeji na kale zenye
kiwango kikubwa cha virutubisho hivyo bila kuathiri ladha za mboga hizo.
Dr Juvik anasisitiza kuwa, dutu hizo huwa hazibaki mwilini kwa muda mrefu kwa hiyo
tunahitajika kula mboga hizo walau kila baada ya siku tatu au nne ili kupunguza uwezekano
wa kupata magonjwa ya moyo, saratani, kisukari na maradhi mengineyo yanayotutesa.
No comments