SIMULIZI:FACEBOOK SEHEMU YA 09

SEHEMU YA 08
ILIPOISHIA.....................
"Nakupenda pia Reshmail umebadili maisha yangu moja kwa moja nina maisha mazuri sasa" alijibu Eva kwa upole huku akimwangalia Reshmail aliyekuwa anaishusha chandarua yake aweze kulala. Ni kweli walitokea kupendana wawili hawa.
"Hivi Resh una mpango bado wa kusomea uhasibu mi lazima niwe mhasibu"
"Mh! unavyojiaminisha utadhani tumefaulu tayari" alijibu Resh.
"He! mi najua sisi kufaulu kwetu sio swali ni jibu,swali ni je tunaenda chuo gani na kusomea nini." alijiaminisha Eveline.
"ok! nilidhani nitasomea uhasibu lakini kwa heshima ya Adam nitasomea sheria" alijibu Reshmail kwa furaha.
"Mh! na upole wako huo na mambo ya kutoa hukumu wapi na wapi? mwenzio naangalia ankara" alisema Eva.
"Wala hata siendi kuhukumiana naenda kwa heshima tu" alisisitiza Reshmail.
"Mh! haya mheshimiwa hakimu napenda kujitetea kama ifuatavyo" Eve alitania akifuatiwa na kicheko kikubwa kutoka kwa Reshmail.
INAENDELEA...............
Maisha yaliendelea vyema sana tu japo yalikuwa maisha ya mashaka Adam aliruhusiwa kuongea na kuuliza kila kitu kasoro swali moja tu "Kwa nini niko hapa?",ndio hakuruhusiwa kuliuliza hata kwa mbali,watu wote pale hawakuwa na ubaya nae hata kidogo,hawakumtesa,hakugombezwa wala hakufanya kazi,alipewa huduma zote za msingi,aliweza kutoka nje na kwenda bustanini lakini nje ya geti hakuruhusiwa. Tayari aliyazoea maisha haya lakini kumbukumbu ya jinsi alivyochukuliwa ndani ya jumba la wakweze bila kupata msaada wowote ule "Nani atakuwa nyuma ya haya yote mlinzi alikuwa wapi? Mama Resh je?" alijiuliza sana bila kupata wa kumpa jibu. "Hivi unaitwa dada nani vile?" Adam alimuuliza dada mmoja ambaye kila baada ya siku tatu alikuja kufanya usafi katika chumba chake."Naitwa Beatrice Cosmas niite Bite" alijibu huku anafuta vioo kwa dirisha la chumba cha Adam. "Una jina zuri wewe mh!"Alisanifu Adam. "Asante wewe ni Adam eeh!" aliongezea yule binti huku akiwa ameacha shughuli yake aliyokuwa anafanya. "Ndio mimi ni Adam! samahani nikuulize maswali machache" "Uliza tu lakini sitakujibu sasa hivi" "Kwa nini?" "We uliza yote ndo nitakwambia kwa nini" "Hivi hapa ni wapi? kwa nani? na kwa nini nipo hapa?" "Ndio hayo matatu tu?...sawa nitakujibu kwa sharti dogo sana yaani" "Sharti gani hilo mi nipo tayari"alitoa uhakika Adam bila hata kulijua sharti lenyewe. "Sikia Adam sina haja ya kuzunguka zunguka nina mwaka wa pili hapa kitu kinaitwa mwanaume katika mwili wangu ni kama ndoto sasa ni wewe wa kutii kiu yangu na mimi nitajibu maswali yako" alijieleza Bite,jambo ambalio lilikuwa zito na la kumshangaza Adam."Mh! au ndo mtego tena kutoka kwa Reshmail? dah! ikiwa hivyo nitaaibika kweli mimi"Alijiwazia Adam kwa mashaka makubwa kabla ya kujibu. "Basi utakuja kunijibu baadaye!" alisema Adam. "Haya usiku na wewe jiandae" alijibu na kuaga Bite. Hayawi hayawi mara yakawa usiku wa saa tatu,Bite tayari ndani ya chumba cha Adam ndani ya khanga moja peke yake. "Haya nipe nikupe hakuna longolongo hapa" alizungumza Bite."Subiri taratibu basi,sikiliza" alianza kujitetea Adam wakati Bite anajisogeza kitandani,Adam alikuwa amechelewa tayari joto la Bite lilipenya katika mwili wake na kumchanganya hadi kujikuta akifanya kinyume na alivyotarajia kwamba atafanikiwa kutegua mtego wa Bite badala yake alikuwa ameshafanya mapenzi na Bite. Kwa Bite ulikuwa ushindi mkubwa sana kwani tangu aletwe hapo kuwa msaidizi wa kazi za ndani ya vyumba hakuwahi kutoka nje ya jengo hilo,sio kwamba alikuwa amefungwa hapana kila kitu kilikuwepo ndani kila siku pia alikuwa ameridhika kuwa hapo. "Hapa ni Iringa,nimejibu swali lako la kwanza tuendelee tena nikujibu swali la pili na tatu" alisema Bite kwa shauku kubwa sana. "Hapana Bite imetosha kwa leo sijisikii vizuri,siku nyingine basi sawa!" alidanganya Adam na Bite hakuwa mbishi akambusu Adam shavuni akajiondokea zake. Ilimchukua takribani siku tano Bite kugundua kwamba tayari ameshika ujauzito jambo ambalo halikuruhusiwa katika jumba hilo na alipewa onyo kali wakati anaingia hapo. Kwa usalama wake na Adam alifikiria suala la kutoroka lakini haya yote aliyafanya baada ya kuongea na Adam na kumweleza hali halisi. Ni katika wasaa huo alimweleza Adam chanzo ambacho kinaweza kuwa kimemsababishia yeye kuwepo pale "Umemchukulia kigogo mpenzi wake,umemendea mtoto wa kizito au umemkataa kimapenzi mtu maarafu" hizo ndizo zilikuwa baadhi ya sababu alizoorodheshewa na Bite,lakini kwake yeye aliona hakuna hata moja inayomuhusu kwani wazazi wote wawili wa Reshmail walimpenda sana hakuwa tayari kuweka hisia kwamba pengine moyoni wanamchukia. "Usijali lakini hutakaa milele humu,huwa unafikaMuda aliyekuweka humu akiridhika unatoka. "Nitamlea mtoto,napenda watoto hata kama usipokuwa mpenzi au mume wangu nitampenda sana na nitamwita....." "Christian akiwa mvulana au Christina akiwa msichana" alidakia Adam ambaye kwa mbali alianza kumtamani Bite kimapenzi.
ITAENDELEA....................................
No comments