• Breaking News

    SIMULIZI YA MAPENZI: SOMA SIMULIZI YA KUSISIMUA -FACEBOOK SEHEMU YA 05




    SEHEMU YA 04

    ILIPOISHIA......................


    "Ungejua hata usingesema wewe twende ukajionee maajabu ya mwaka" alijibu Adamu huku pikipiki ikizidi kushika kasi.
    Ndani ya dakika tano tayari walikuwa Nyegezi kona ambapo Huha alipaki pembezoni kidogo na barabara iendayo stendi kuu ya Nyegezi jijini Mwanza,Adam alielekea dukani kununua vocha,na Huha akasogea pembeni kidogo aweze kuvuta sigara yake.

    USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA 



    INAENDELEA.................

    Dereva akiwa mwingi wa mawazo yake binafsi yasiyomuhusu Reshmail wala Eve na hata kama yangekuwa yanawahusu ule haukuwa muda muafaka wa kuwaambia.Macho ya Reshmail yalikuwa yamekutana na bango kubwa lililoandikwa "KARIBU CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AUGUSTINO" kwa hamu kubwa aliyokuwa nayo ya kumwona Adam ambaye alikuwa pia mwanafunzi ndani ya chuo hicho ndio sababu kuu ya kujikuta akipiga kelele kwa nguvu hali iliyomshtua dereva kutoka katika mawazo mazito na kujikuta akiyumbisha gari huku na huko hadi ilipokutana na pikipiki iliyokuwa imepakiwa pembezoni mwa barabara na kuirusha umbali ambao si wa kutisha sana,iligeuka vurumai madereva wa teksi na bodaboda za pikipiki walikuwa wakali sana hawakutaka kusikia la mtu,wengine hasira za kukosa abiria tangu waingie kijiweni asubuhi walizihamishia katika tukio hilo. Usingekuwa upole wa yule dereva basi mawe waliyobeba wananchi yangeigeuza ile gari kuwa mkweche. Eveline alitelemka garini kwenda kumsaidia dereva kujitetea lakini Reshmail uoga ulimtawala akawa amejibana kwenye viti vya nyuma vya ile gari huku akitetemeka.

     "Mh! Adam hawezi kukosa mwenyeji maeneo haya ngoja nijaribu kumpigia,ah! hii safari imetawaliwa na mikosi dah!" aliwaza Resh huku akichukua simu yake kutoka katika kipochi chake.
    Lakini kelele zilizokuwa pale aliamini hawezi kusikilizana vizuri na upande wa pili,taratibu huku akitetemeka alifungua mlango akashuka na kuanza kutembea kuelekea pahali ambapo kidogo pametulia. 

    Zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wenye hasira eneo lile wakageuza vichwa vyao kuangalia kazi ya Mungu ilivyotendeka vyema katika mwili wa Reshmail,badala ya kumpigia kelele dereva,miluzi mikali ikiongozwa na dereva mkongwe wa teksi eneo lile ndugu Sanya Bonda ikahamia kwa Reshmail,Resh akajifanya kama hasikii vile "Ilikuwa haki ya dereva kupotea njia jamani" Bonda alisema kwa sauti ya juu na kugeuza hasira za watu kuwa vicheko. Resh taratibu akaufikia mti mdogo mbali na eneo la tukio akabonyeza namba za Adam. Simu iliita muda mrefu bila kupokelewa. Alipopiga mara ya pili simu ilipokelewa."Helow Resh subiri nisogee pembeni nakupigia kuna tatizo limenipata" alijibiwa na Adam katika simu.

    "Hata mi....." kabla hajamalizia kauli yake Reshmail simu ilikatwa akiwa bado anaduwaa kama dakika mbili pembeni yake alizengea kijana mmoja ambaye Resh hakutaka hata kumwangalia machoni,alijua ni walewale waliokuwa wakipiga miluzi na kumwita majina waliyotaka. Resh taratibu akajisogeza pemben.

    "Vipi dada mbona wanikimbia au mi nanuka halafu we mrembo haya basi umebarikiwa sana najua unataka kusifiwa" aliongea yule kijana lakini Resh hakujibu.

    Simu yake ya mkononi iliyokuwa katika mfumo wa kimya(Silence mode) ilikuwa inatoa mwanga kuashiria aidha kuna ujumbe umeingia au kuna simu inaingia,lakini kwa jinsi alivyoandamwa na yule kaka kwa maneno hata hakuweza kugundua.

    Baada ya dakika kadhaa akaondoka yule kaka ndipo kuangalia simu akagundua ilikuwa imeita mpaka imekata na hakuwa mwingine bali ni Adam alikuwa amepiga,harakaharaka akapiga tena. 

    Ulikuwa mshangao wa hali ya juu sana Reshmail hakuamini alipomwona yule kijana aliyekuwa ametokea pale dakika chache zilizopita kuelekea kwenye zile vurugu ndio anapokea simu."Resh mbona nimekupigia hupokei mamaa" alimshuhudia yule kaka akiongea kwenye simu huku akirejea lile eneo kukwepa kelele,kama ilivyo kwa mtu aliyenaswa na umeme Reshmail alikuwa ametulia tuli na simu sikioni huku yule kaka akizidi kulikaribia eneo lile “Reshmail mbona huongei!!” aliendelea kuuliza bila kupata majibu.

    "Adam" alijitutumua Resh na kutamka akiwa jirani naye kabisa,bila kujua yule kijana akaangusha simu yake hakuamini msichana aliyetoka kuongea nae dakika kadhaa ndio Reshmail wa Arusha.

                                   ***
    Vurumai lilisawazishwa haraka sana Adam na Huha ndio waliokuwa wamiliki wa ile pikipiki iliyogongwa na gari waliyokuwemo akina Reshmail."Jamani huyu hapa ni dada yangu,ndio alikuwa amenipigia simu tuonane hapa naomba haya mtuachie sisi" Adam aliuambia umati ule ambao hasira zao zilikuwa zimeanza kupoa na haraka walimwelewa wakaacha kumzonga dereva.

    Reshmail bila kupoteza muda akamwongoza Adam wakaingia garini akampa pesa taslimu shilingi laki tatu kwa ajiri ya matengenezo ya ile pikipiki naye Adam akamkabidhi Huha kisha akajumuika na Eve pamoja na Reshmail katika gari,huku Reshmail akiwaacha watu hoi kwa uzuri wake wa asilia ambao hata Adam alikuwa amechachawa nao na kukubaliana na ukweli kwamba picha zilizotumwa zilikuwa za Resh kweli.

                                ***
    Bi Gaudensia alifika Dar-es-salaam majira ya saa tatu usiku,bado alikuwa hajaridhika kumaliza siku yake bila kuongea na mwanae,hivyo punde tu baada ya kuingia chumbani mwake aliamua kujaribu kupiga namba za simu za Reshmail ambazo zilikuwa hazipatikani siku nzima. Furaha aliyoipata ilikuwa haisimuliki,pale simu ilipoita upande wa pili"Mh! kalala nini huyu?" alijiuliza simu ilivyoita kwa muda mrefu bila kupokelewa,lakini mara ikapokelewa

     "Helow! samahani Reshmail amelala" sauti ya kiume ilijibu baada ya kupokea kisha simu ikakatwa na kuzimwa. Mama Resh hakuamini kuwa amesikia sauti ya kiume katika simu ya mwanae alidhani amekosea namba lakini alipohakikisha zilikuwa zenyewe,wivu mkali ukamshika,akajaribu kupiga mara nyingi lakini bado hali ilikuwa ileile simu ilikuwa imezimwa usingizi ulipaa,alitokwa na jasho,hisia mbaya zikamvuruga na kufanya kichwa chake kiume sana,mama huyu alikuwa amejisahau kabisa kuwa Reshmail ni mwanae wa kumzaa, alizurura kama mtu anayetafuta kitu ambacho amesahau alipokiweka pale chumbani,alitamani kupiga kelele lakini aliamini hazitasaidia kitu.

                                     ***
    Reshmail akiwa usingizini Adam pembeni yake,yeye(Resh) alikuwa hoi kwa uchovu wa safari na misukosuko yote waliyopitia,na alipomaliza kuoga tu na kupata chakula alisinzia,hata simu yake ilipoita hakuisikia hata kidogo na hata angeisikia asingeweza kunyanyuka kupokea "Resh ni kipetito anapiga" Adam alimuuliza Resh aliyekuwa hoi kitandani."Ah! ni rafiki yangu mwambie nimelala" alijibu kwa taabu akiwa hata hajui anachokiongea. Naye Adam bila kugundua kwamba Resh hajui anachokisema na ile namba ni ya mama yake Resh alipokea na kuzungumza

    USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA


    Kitendo cha Adam kumkuta Reshmail akiwa bado ni bikra kilimzuzua sana,mapenzi yake kwa Halima yalipungua sana na kuisha kabisa hatimaye. Siku tatu mfululizo walizotumia pale Millenium Hotel zilitosha kuvunjilia mbali penzi la Adam na Halima na kujenga penzi imara kati ya Adam na Reshmail.
    "Mwezi wa pili uje ujitambulishe nyumbani Adam yaani siwezi kusubiri kwa kweli nakupenda Adam wewe ni mwanaume wangu wa kwanza na ninakuahidi nitajitunza kwa ajili yako" Reshmail alikuwa anamsisitiza Adam siku alipokuwa amewasindikiza uwanja wa ndege tayari kwa wawili hawa kurejea Arusha shuleni.

    "Mama anapiga! Eve" Resh alimwambia Eve pale simu yake ilivyoita."He! usiniambie huyo ndio mama,sasa mbona ulikubali niongee nae usiku ule? aliduwaa Adam.

    "Eti! uliongea nae? Yesu wangu!" alishtuka Resh lakini Eve akamshauri azime simu kwanza mengineyo watajua mbele kwa mbele naye Resh akatii amri hiyo haraka akaizima simu bila kupokea Resh kwa kiasi kukuwa alikuwa amemzoea na kumwamini Eve.

    Adam,Resh,na Eve waliagana kama watu waliofahamia na kukaa pamoja siku nyingi sana,Resh alimkumbatia Resh alimkumbatia Adam kwa muda mrefu hadi Eve alipowatenganisha na kuambiana Kwaheri.

    USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA

    ***

    Ilikuwa imebaki miezi minne wafanye mtihani wa kumaliza kidato cha tano,Resh akiwa amekolea katika penzi la Adam na kusahau kuhusu
    Mama yake ambaye alikuwa amezuiwa na mwanaye huyo kwenda pale shuleni kumsalimia kwa madai kwamba yeye(Reshmail) anataka ajikite zaidi katika masomo. Reshmail kwa maksudi akabadilisha namba yake ya simu ili mama yake asiweze kumpata mara kwa mara badala yake muda mwingi akawa anawasiliana na Adam.

    Mwezi wa pili ilikuwa ni likizo ya mwezi mzima kwa wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita na pia wakati huohuo wanafunzi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino huwa katika mapumziko mafupi baada ya kumaliza muhula(Semister) ya kwanza. Kwa Reshmail ulikuwa wakati muafaka wa kumtambulisha Adam kwa wazazi wake jambo ambalo aliamini lingesaidia kupunguza makali ya mama yake. Tangu akiwa mtoto kamwe hakuwahi kuwakwaza wazazi wake kwa sababu ya wanaume hata siku moja hivyo alitegemea hawatampinga.

    Ilikuwa siku ya furaha kubwa sana kwa Bi. Gaudencia na familia yote kwa ujumla kumwona tena Reshmail nyumbani baada ya miezi mingi tena akiwa mwingi wa furaha. Lakini tofauti na mama yake alivyofikiria kwamba mwanae huyo anafurahia kurudi katika ulimwengu wao wa mapenzi haramu yeye(Reshmail) alikuwa anafuraha ya kumtambulisha Adam ndani ya siku chache.

    Kwa kujua wazi kabisa mama yake atachukizwa na maamuzi yake hayo,Reshmail aliamua kulifikisha hilo mbele ya Mzee. Manyama ambaye ni baba yake.

    "Kwa sababu ni uchumba tu na hakupeleki popote hamna tatizo hata kidogo,mlete tu mwanangu mlete una maamuzi mazuri sana sio kama wasichana wengine wanafanya upuuzi kimyakimya mambo yanapokuwa mabaya ndio wanasema" alijibu mzee.Manyama huku akimshika mwanae huyo shavuni,Resh akatabasamu na kumkumbatia baba yake "I love you dad(Nakupenda baba)" Resh akamwambia kwa furaha tele mzazi wake huyo,huku moyoni akijiaminisha kwamba hapatakuwa na kikwazo tena kwa mama yake kwani baba ndiye kichwa cha familia.

    Baada ya siku tano Adam aliwasili ndani ya kasri la mbunge huyu.Alikuwa anaogopa na hakuamini kama angepokelewa na kama angepokelewa alijua yatakuwa mapokezi mabaya sana kwani katika simulizi mbalimbali anazozisikia kwa watu zilimwonyesha kwamba ni vigumu sana kwa wazazi kumwelewa mtoto wa kike linapokuja suala la kumtambulisha mwanaume kama mchumba wake.

    "Da Rosemary nina hofu mie" Adam alimwambia dada yake kipenzi waliyekuwa wameongozana naye "Acha uoga bro mbona hata sisi babu yetu alikuwa chifu?

     kwani chifu na mbunge nani zaidi" alitania Rosemary kumwondoa hofu kaka yake.Mapokezi waliyoyapata kutokea kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo yaliwashangaza mno waliwakuta watu wa kuwapokea na kwenda nao kwenye gari mbili walizokuja nazo,waliwafikisha hadi getini ambapo kina dada wawili kwa heshima kabisa waliwaongoza hadi sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao,japo usoni waliuficha mshangao wao lakini moyoni uliwajaa tele.

    Adam akiwa ndani ya suti nyeusi wanazotumia wanasheria katika shughuli zao na Rosemary aliyevaa suti pia walielekezwa wapi walipo wazazi wa Reshmail wakaenda kutoa salamu zao,ilikuwa ni hafla kubwa sana ndugu,jamaa na marafiki wapatao miamoja walikuwa wamealikwa na mheshimiwa huyu. Ilikuwa kama harusi kwa asiyejua lakini ulikuwa utambulisho tu.

    Bwana na bibi Manyama walipendeza kwelikweli na walikuwa na kila haki ya kuitwa wakwe na Adam. Furaha ya Bi. Gaudencia ilificha chuki aliyokuwa nayo moyoni dhidi ya Adam kwa kumchukua mwanae ambaye ndio alikuwa anampa raha zote za dunia.

    ITAENDELEA KESHO.........................

    USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA




    No comments

    Post Top Ad