• Breaking News

    SIMULIZI: FACEBOOK SEHEMU YA 08



    USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA


    ILIPOISHIA

    "Narejea shule kesho" kwa msisitizo na tabasamu alijibu Reshmail. Mzee Manyama hakuamini kwani alikuwa akiwaza ni namna gani atamshawishi mwanae aweze tena kurejea shuleni baada ya matatizo yote yaliyojitokeza kwa mchumba wake Adam ambaye hadi wakati huo bado mwili wake ulikuwa haujapatikana wala taarifa yoyote zaidi ya nguo zikiwa na matundu ya risasi na damu."asante sana mwanangu nakupenda sana" mzee Manyama aliongea kwa furaha huku akimkumbatia mwanae.


         Tangu kupotea kwa Adam aliyehisiwa kuwa tayari amekufa kulipokelewa kwa hisia tofauti na wananchi huku asilimia kubwa ikiegemea upande wa imani potofu za kishirikina wakihusisha tukio hilo na utajiri alionao Mh. Manyama na uchaguzi uliokuwa mbele yake.
    INAENDELEA...

    "Wamemtoa mwanangu kafara ili waongeze utajiri,nilimwambia Adam aoe msukuma mwenzake ona sasa,watoto wa siku hizi wabishi wanajifanya wanajua sana na elimu yao inawadanganya" mama yake Adam alikuwa analaani vikali mbele ya mume wake wakiwa ndani ya nyumba yao maeneo ya Igoma kwa 'one-way'
    "Usiseme hivyo mama Adam kumbuka sisi ni wakristu,tumwachie Mungu yeye ndio atajua nini cha kufanya" Babaye Adam alimtuliza mkewe huku akimgongagonga mgongoni kwa kutumia kiganja cha mkono wake wa kuume.
    Mawasiliano baina ya familia hizi mbili ya Adam jijini Mwanza na ya Reshmail jijini Dar-es-salaam yalikuwa yamekatika licha ya baba yake Adam (mzee Michael) kutangaza kuwa kutoka moyoni mwake amesamehe yote yaliyotokea na anaamini ni mipango ya Mungu lakini kinyongo kilionekana dhahiri kwa matendo,upendo wa zamani haukuwepo tena jambo hilo lilimfadhaisha sana mzee Manyama kiasi cha kukondeana na kukosa umakini katika utendaji wake wa kazi jambo lililoishusha sana heshima yake kama mbunge aliyekuwa anaheshimika sana kuanzia bungeni hadi jimboni kwake,wapinzani walitumia fursa hiyo kumchafua hasahasa na kweli uchafu huo ukakubalika kwa wananchi kwa ujumla Manyama hakuwa na lake tena pale,wananchi walimpuuzia sana tofauti na zamani na hata hiyo miaka miwili iliyobaki wananchi waliiona kama ni mingi sana kuwa na kiongozi wa aina yake.
    Kuliko fedheha yote hiyo Mh. Manyama kwa hiari yake mwenyewe alipitisha kura ya maoni ya wananchi kuhusu imani waliyonayo kwake kama mbunge wao. Asilimia 70 ya waliopiga kura walidai hawana imani naye huku asilimia kumi na nne tu ndio wakidai bado wana imani naye na kura zilizobaki zikiharibika,rasmi Manyama akawa ametolewa bungeni na katika uchaguzi mdogo uliofanyika akachaguliwa mbunge kutoka chama cha upinzani na maisha yakaendelea huku Mh.Manyama akiendelea na biashara zake mikoani.
                                 * **
    Adam akiwa pale bustanini alivamiwa ghafla na wanaume wawili wa shoka wakiwa na bunduki,ishara ya kidole mdomoni ilimfanya atulie tuli kisha wakamwonyesha ishara kwamba awafuate alifanya kama walivyotaka hadi kwenye gari iliyokuwa imepaki pembeni kidogo ya nyumba yao Adam alishangazwa sana na ukimya uliokuwepo hakuwepo mlinzi wala mama mkwe wake.Safari yao ilikwenda mpaka Iringa gari iliyokuwa na vioo vyeusi 'tinted' ilimzuia Adam kujua ni wapi alipo,gari ilizimishwa ndani ya jumba kubwa sana ambapo alipelekwa kwenye chumba kikubwa tu,hofu kubwa ilimtawala hakujua kwa nini yuko pale,hakupigwa wala kupewa bughudha yoyote,hali hiyo ilzidi kumshangaza "au ndio wachuna ngozi" alijiuliza Adam kwa hofu tele.
    Hayo ndio masharti ambayo mama Reshmail alitoa kwa vijana aliowapa tenda hiyo ya kumtorosha Adam pale nyumbani. Shida yake haikuwa kumtesa Adam bali kumweka mbali na mwana (Reshmail) ambaye alikuwa amempagawisha ipasavyo katika mapenzi ya jinsia moja.Suala la pesa halikuwa tatizo hata kidogo alichohitaji ni kutimiziwa alichotaka. Mkataba wa miaka mitano ndio alioingia na watu hawa kukaa na Adam bila kumruhusu kutoka nje ya jingo.Bi Gaudencia aliamini kwamba kwa kutokomea Adam mbele ya uso wa Reshmail ilikuwa fursa nzuri ya kurudisha tena uhusiano wake na Reshmail ambao ulikuwa unaelekea kufa lakini kinyume chake alikuwa ameibua chuki kubwa baina yake na mwanae “heri  wote tukose kama ni hivyo” alijiapiza mama Reshmail baada ya kuona dalili za kumshawishi Reshmail hazipo tena
           Alikuwa ni Reshmail mwingine kabisa mkasa uliomkumba ulimbadilisha sana na kuitanua akili yake sana,Eveline naye alisikitishwa na yaliyomkumba shoga yake akajitahhdi sana kuwa karibu naye kumpa moyo huku akijiepusha sana kufanya vitendo ambavyo vitamkumbusha Resh jinsi alivyoweza kukutana na Adam. Ni katika kujiepusha na kumkera rafiki yake huyo kipenzi Eveline akajikuta amefuta picha za uchi na filamu za ngono katika kompyuta yake akawa si mtu wa kutoroka shule,hakuwa tena mtu wa wanaume na hatimaye akawa Eveline wa kuigwa na wanafunzi wenzake jambo hilo liliwaduwaza sana wanafunzi pale shuleni lakini ndio hivyo Eve alikuwa amekubali mabadiliko katika maisha yake. Juhudi zao katika masomo ziliendelea kuwaweka katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri mtihani wao wa mwisho. Hawakuyazungumzia tena yaliyopita tena walijadili mapya na yanayowanufaisha "Eveline wewe ni kama dada yangu nakupenda sana"
    "Nakupenda pia Reshmail umebadili maisha yangu moja kwa moja nina maisha mazuri sasa" alijibu Eva kwa upole huku akimwangalia Reshmail aliyekuwa anaishusha chandarua yake aweze kulala. Ni kweli walitokea kupendana wawili hawa.
    "Hivi Resh una mpango bado wa kusomea uhasibu mi lazima niwe mhasibu"
    "Mh! unavyojiaminisha utadhani tumefaulu tayari" alijibu Resh.
    "He! mi najua sisi kufaulu kwetu sio swali ni jibu,swali ni je tunaenda chuo gani na kusomea nini." alijiaminisha Eveline.
    "ok! nilidhani nitasomea uhasibu lakini kwa heshima ya Adam nitasomea sheria" alijibu Reshmail kwa furaha.
    "Mh! na upole wako huo na mambo ya kutoa hukumu wapi na wapi? mwenzio naangalia ankara" alisema Eva.
    "Wala hata siendi kuhukumiana naenda kwa heshima tu" alisisitiza Reshmail.
    "Mh! haya mheshimiwa hakimu napenda kujitetea kama ifuatavyo" Eve alitania akifuatiwa na kicheko kikubwa kutoka kwa Reshmail.


    ITAENDELEA.............................


    USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA


    No comments

    Post Top Ad