PROGRAMU YA SIMU YA UZAZI WA MPANGO,NJIA YA ASILI.

Matumizi ya kupanga uzazi kwa njia ya kalenda yaweza kuwa na ugumu kufuatilia wakati mwingine kutokana na majukumu mbali mbali ya kimaisha. Programu za simu (mobile apps) zaweza kutumika na kukurahisishia na kuweza kutumia njia ya kalenda kwa usahihi.
CycleBeads® ni programu ya simu zinazotumia mfumo waAndroid na hutumika kusaidia wanafamilia kupanga uzazi. Programu hii imebuniwa na idara ya afya ya uzazi katika chuo kikuu cha Georgetown na imetengenezwa maalum ambayo ni rahisi kutumia na ya uhakika kwa kina mama kupanga na kuzuia ujauzito kwa kutumia njia ya
Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa njia hii imeweza kuwa na usahihi wa zaidi ya asilimia zaidi ya 95 hii
ikiwa ni sawa au zaidi ya njia nyinginezo zitumikazo kuzuia ujauzito.

Sharti la kitabibu la kutumia programu hii ya simu za android ni kuwa mwanamama awe na mzunguko wa hedhi wa kati ya siku 26 hadi 32 . Inakadiriwa kuwa 80% ya kinamama wote huwa kati ya siku hizo zilizotajwa. Endapo mwanamama atakuwa na mzunguko wa hedhi katika mwaka ambao ni pungufu ya siku 26 au zaidi ya siku 32,
programu hii haitakuwa na ufanisi. Kama hauna uhakika na mzunguko wa hedhi inabidi uanze kufuatilia kwa kuweka rekodi kabla ya kuanza kutumia programu hii. Kama umejifungua karibuni au ulikuwa unatumia njia za homoni za uzazi wa mpango inabidi usubiri hadi pale mzunguko wa hedhi utakapokuwa umerudi kawaida(kati ya siku 26 hadi 32 za mzunguko wa hedhi),kabla ya kutumia programu hii.
Baada ya kupakua na kusimika programu hii katika simu yako, mwanamama huitajika kuingiza tarehe ambayo alianza kuona siku zake za hedhi, na programu hii humuonyesha siku zilizo salama na zile ambazo mwanamama anaweza kupata mimba.
Waweza kupakua programu ya CB kutoka google play store au tembelea mtandao wawww.cyclebeads.com kwa maelezo zaidi.
No comments