• Breaking News

    HADITHI: SOMA SIMULIZI YA KUSISIMUA -FACEBOOK SEHEMU 01


    “"Reshmail Manyama want to be your friend.'confirm' 'ignore' ulikuwa ni ujumbe ambao macho yangu yalikutana nao nilipofungua mtandao wa kijamii wa ‘facebook’,sikumbuki kama nilijifikiria mara mbili kwani niliona ni jambo la kawaida sana kukutana na 'notifications’ kama hizo,na mara zote neno confirm(kubali) lilipata fursa ya kutumika.hivyohivyo hata kwa Reshmail nilifanya hivyo."You and reshmail are now friends" ndio ujumbe ulionisindikiza baada ya kukubali ombi lile kutoka kwa Reshmail.

                                 *   *  * * *
    Ni kijana mtanashati niliyebahatika kukutana nae pale chuo kikuu cha mtakatifu Augustine Mwanza,alijipenda kuanzia ndani ya chumba chake hadi mwili wake,ilikuwa ni nadra sana kumfumania akiwa amevaa nguo aliyoivaa jana,bila kumnyima haki yake nasema alikuwa anapendeza kila siku,macho yangu ya kipelelezi na kamera zangu za kipaparazi kamwe hazikufanikiwa kumjua aliyekuwa ubavu wa pili wa bwana huyu yaani 'MPENZI'. Ukipenda waweza kuniita kimbelembele lakini ukiniita hivyo basi majina hayo yatakuwa mengi pale chuoni kwani wengi walikuwa na shauku kubwa ya kujua siri hiyo na kamwe hawakufanikiwa.

    Binadamu hatuna dogo watu washaanza kusema eti huenda jamaa ana matatizo makubwa tu mwilini mwake ndio maana yuko peke yake licha ya kushobokewa na wasichana warembo, mh! mimi sikuwa mmoja wao lakin nilijiuliza pia kulikoni?? 

        Makala mbovu zilizokuwa zinaandikwa na gazeti la chuo lililojulikana kama ‘Saut voice’ ndo zilinizonivuta zaidi kutaka na mimi siku moja kuandika katika gazeti hilo lililokosa mvuto siku za hivi karibuni makala nzuri itakayorudisha heshima ya gazeti hilo.Taratibu nilijenga mazoea na hatimaye nikafanikiwa kumzoea "THE MOST WANTED" ucheshi wangu ndio uliomvutia zaidi kupenda kuwa karibu nami pamoja na mchezo wa mpira wa miguu kwani wote tulikuwa mashabiki wakubwa,haukupita mwezi mzima nikawa nina uwezo wa kuanza kazi yangu,ni mimi na Adam Michael kwenye meza moja chumban kwangu ananipa hadithi yake ya maisha yaliyomfanya awe kama alivyo.

    "Aah!! jamani Reshmail..." alianza Adam,yangu masikio na macho nikaanza kusikiliza kwa makini.

                         **        **          **
        Hadi anafika mwaka wa pili kimasomo chuoni mtakatifu Augustine Mwanza kitivo cha sheria Adam aliitumia simu yake ya mkononi kwa ajili ya kupiga,kutuma ujumbe (sms) na kupokea ni hayo tu na kwa upande wa pili alipenda sana kucheza michezo ya simu (game) ya kwenye simu.

        Alikuwa ni Hughorito Hamada ama maarufu kama 'HUHA'.hakuwa tu rafiki yake adam bali pia alikuwa ni mshirika wake wa chumba (room mate) na pia walisoma darasa moja la sheria pale chuoni,ni huyu aliyemuingiza Adam katika ulimwengu ambao hatausahau kamwe,tabia yake ya kupenda kuazima simu ya Adam aina ya Nokia Express music kwa dhumuni la kuchat katika mtandao maarufu wa kijamii wa ‘facebook’ ndio ilimshawish Adam naye kuanza kujiuliza kulikoni hasahasa alipokuwa anamwona Huha akicheka mwenyewe kila anapokuwa anachat,"Mh! we jamaa yangu chizi kweli yaani unacheka na watu usiowaona" Adam alimkebehi Huha alipokuwa anacheka na simu yake punde tu baada ya kuanza kuchat

    "Kwani we ukiwa unaota unaongea huwa kuna watu mbele yako?" Huha alijibu mashambulizi na Adam akabaki kimya na taulo yake kiunoni akaenda bafuni kuoga.

    "Mwanangu nimekuunga na wewe namba yako ya siri ni..,.." hata kabla Huha hajamaliza adam akamkatisha "Nini? huo upumbavu wako sitafanya kamwe bro" ..."Hv kwan inakuwaje huo upuuzi" Adam akajikuta anauliza baada ya kuwa amevaa nguo zake "Hii kitu inaitwa FACEBOOK,yan adam ukijiunga wewe hutoki na utakuwa nayo bize kweli" Adam alisikiliza kwa makin japo alijidai kufanya dharau machon,Huha hakujali aliendelea kutoa somo had Adam akapata mwanga,"Mh. Sidhan kama itanivutia bt i wil try". Alijisemea adam wakat anachukua simu yake.

    ITAENDELEA.........................

    USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA 

    No comments

    Post Top Ad