• Breaking News

    Baby Madaha: Hatukurupuki, tunafanya kweli

    madaha

    Mwanadada anayeunda Kundi la Scorpion Girls, Baby Madaha amefunguka kuwa, yeye na wenzake Isabela Mpanda na Jini Kabula wanapoamua kufanya kazi huwa hawakurupuki bali wanajipanga kisha kutoa kitu ambacho kitasumbua kwenye gemu.
     Akipiga stori na safu hii, Baby Madaha alisema kuwa, waliamua kulihuisha kundi lao hilo na kuamua kuja na ngoma yao mpya waliyoipa jina la Marioo wakijua ni wimbo ambao utashika na kichupa chake kitakuwa balaa.
    “Audio iko tayari, sasa hivi tunafanyia kazi video, kwa kifupi tumeamua kuleta mapinduzi kwenye gemu na kwa sapoti kubwa tunayopata kutoka kwa Mama Loraa, tunaamini kundi litabamba,” alisema Baby Madaha.

    No comments

    Post Top Ad