• Breaking News

    Rais MAGUFULI awataka watanzania kumuenzi SOKOINE kwa uadilifu


    Rais Dkt. JOHN MAGUFULI amewataka watanzania kuenzi misingi ya uadilifu iliyowekwa na aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka 1984.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea 
    machache wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam
    Rais MAGUFULI amesema hayo wakati  wa ibada ya kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo cha EDWARD MORINGE SOKOINE pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na Madhehebu ya Dini.     
    Kwa upande wao Rais Mstaafu wa awamu ya TATU, BENJAMIN MKAPA na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la DSM, MWADHAMA POLYCARP, KARDINALI  PENGO wameelezea mchango wa Hayati SOKOINE katika maendeleo ya taifa wakihusisha utendaji wake na jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuharakisha maendeleo ya taifa.        
    EDWARD MORINGE SOKOINE alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa vipindi viwili tofauti kati ya mwaka 1977 na 1980 ambapo aliongoza tena kati ya 1983 na 1984 alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 46.      
    Huko, MOROGORO katika eneo la WAMI DAKAWA ilipotokea ajali iliyosababisha kifo cha hayati EDWARD SOKOINE juhudi za ujenzi wa shule ya kumbukumbu ya SOKOINE zimezidi kufifia kutokana na kutokamilika kwa ujenzi wa shule hiyo.

    April 13, 2016
    MBOZI KATALA

    No comments

    Post Top Ad